HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO
TANGAZO LA MKUTANO MAALUMU WA BARAZA LA MADIWANI LA BAJETI TAREHE 15-16 FEBRUARI, 2018
Kutakuwa na Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kujadili na kupitisha mapendekezo ya Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Chato kwa mwaka 2018/2019 siku ya Alhamis terehe 15 na Ijumaa tarehe 16 Februari, 2018.
Mkutano huo ni Maalumu kwa ajili ya kujadili na kupitisha Mapato na Matumizi ya mwaka 2018/2019 pamoja na Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2018/2019.
Mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri kuanzia saa 4.00 asubuhi kwa siku zote mbili.
Mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ni wa wazi, wananchi wote mnakaribishwa kuhudhuria na kusikiliza.
Limetolewa na
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji
CHATO
14 Februari, 2018
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.