Akiongea na Wananchi hao Mhe. Mkuu wa wilaya ya Chato Eng. Deusdedith Katwale amewataka wafugaji kuachana na tabia ya kufuga mifugo mingi na isiyonatija bali kufuga mifugo michache na ambayo mfugaji mwenyewe utanufaika nayo.
Aidha ameongeza Mhe. Katwale kwa kusema "mifugo hii tunayofuga ilete chachu na kubadili hali ya maisha yetu katika jamii zetu na Serikali kwa ujumla na siyo kuwa chanzo cha kuleta migogoro na uhasama katika maeneo yetu" mfano Nchi kama ya Namibia ina ng'ombe elfu 4 tu lakini ni nchi ya pili Africa kwa kusafirisha Nyama ikiongozwa na Botswana lakini je tujiulize sisi kama wana Iparamasa na taifa kwa ujumla ukiambiwa utafute ng'ombe elfu 4 si unawapata ndani ya Mkoa mmoja au pengine hata wilaya moja tu! sasa hao ng'ombe wote wana tija gani kwa wana Iparamasa na taifa kwa ujumla.
Katika hatua ingine Mhe. Katwale amewapongeza wananchi wa Kata ya Iparamasa kwa namna ambavyo wamekuwa msitari wa mbele katika kusimamia miradi ya Serikali mfano Ujenzi wa Madarasa katika Shule, Ujenzi wa Miundombinu katika vituo vyetu vya kutolea Afya na Miradi ya Maji.
Kwa upande wake Mhe. Diwani wa Kata hiyo amemshukuru Mkuu wa wilaya kwa kukubali na kuitikia wito na kufika katka kijiji cha Ipalamasa kwa ajili ya kuja kutembelea Miradi mbalimbali ya Maendeleo ndani ya Kata, hata hivyo Mhe Diwani amemwomba Mhe. Katwale kuona umhimu wa kuanza kutoa huduma katika kituo cha Afya Ipalamasa.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Kilimo na Mifugo Ndg. Edgar Kimaria akiongea na wananchi wa Iparamasa kwa nyakati tofauti kabla ya uzinduzi wa Josho hilo amewakumbusha wakulima umhimu wa kutumia mbolea ya samadi ili kuendelea kurutubisha ardhi kwa ajili ya shughuli za kilimo kwani ardhi hii imelimwa miaka mingi hivyo kuna baadhi ya virutubisho vimeanza kupungua sasa niombe " achaneni na tabia ya kuchoma samadi hiyo bali pelekeni shambani kwani ni mbolea inayopatikana bila gharama katika maeneo yetu na sisi kama wana Iparamasa kwa takwimu ni kata ambayo inaongoza kwa kuwa na mifugo mingi hivyo hata samadi upatikanaji wake ni wa kutosha"
Akihitimisha shughuli hiyo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Iparamasa amemshukuru sana Mhe Mkuu wa wilaya kwaniaba ya wananchi kwa kukubari wito wa kuja kuwafungulia Josho hilo hata hivyo amemuomba asisite kufika katika kijiji chao mara na wakati mwingine watakapo mwita.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.