Afisa Afya wilaya ya Chato Bi Fransisca Charles ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Usafishaji na Taka Ngumu amewasisitiza watendaji wa Kata, Vijiji, Ma Afisa Afya na Wahudumu wa Afya ngazi ya Kata na Vijiji kuhakikisha wanakuwa msitari wa mbele katika kuhakikisha Chato inakuwa safi na yenye vyoo bora kitu ambacho kitaifanya Chato kung'ara na kuonekana katika mkoa na taifa kwa ujumla.
Aidha akiongea na washiriki wa kikao hicho kutoka katika kata za Mganza, Bwongera, Nyamirembe, Chato Muungano, Katende, Ichwankima, Kigongo na Bukome Bi. Fransisca amekipongeza kijiji cha Mlimani kwa kufanya vizuri miaka miwili mfululizo hasa katika utoaji wa takwimu sahihi na uwepo wa vyoo bora pamoja na kuwa na mazingira safi.
" vyoo bora ndugu zangu ndio msingi wa kulinda jamii zetu dhidi ya magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, kuhara na kutapika"
Afisa Maendeleo ya Jamii Ndg. Tagaya akiwawasilisha mada ya uandaaji wa Mpango kazi ngazi ya Kata juu ya uwasilishaji wa Taarifa kwa asilimia 100 na ufatiliaji na ujenzi wa vyoo bora katika kata angalau asilimia 50 kufikia tarehe 1 Julai 2023
Washiriki wakiwasilisha Mipango kazi waliyoiandaa juu ya utelelezaji wa Mradi wa WASH ambao unahusika na uboresha wa vyoo bora katika vituo vya kutolea huduma za Afya walau asilimia 50 na utoaji wa taarifa asilimia 100 ifikapo Julai 1, 2023 wameahidi kwenda kuusimamia mipango hiyo waliyojiwekea katika kata ili kuleta tija na matokeo chanya kwa Halmashauri na taifa kwa ujumla dhidi ya mapambano ya magonjwa ya mlipuko yatokanayo na uchafuzi wa mazingira.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.