Askari wa Jeshi la akiba kutoka kata zote 23 za majimbo ya Chato Kusini na Kaskazini wanaotarajiwa kusimamia zoezi zima la uwepo wa amani na usalama wa vituo vya kupigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, 2025, walipewa mafunzo ya maadili pamoja na uelewa mpana dhidi ya Uchaguzi huo ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu zilizowekwa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi huku amani na utulivu vikipewa kipaumbele.
Mafunzo hayo ya siku 2 yalifanyika Septemba 18 - 19, 2025 kwa kupita kitarafa yakiongozwa na Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Geita ACP Nestory Didi aliyeambatana na viongozi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Chato,Polisi kata wote wa tarafa husika pamoja na Maafisa wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo Ndg. Philip George wa Jimbo la Chato Kaskazini na Ndg. Berino Msigwa wa Jimbo la Chato Kusini waliotoa Semina elekezi kwa askari hao wa Jeshi la akiba juu ya masuala ya Uchaguzi Mkuu 2025.
ACP Didi aliwataka askari hao kutumia zaidi busara wakati wakutatua changamoto zitakazojitokeza, Kudumisha amani ya ndani na nje ya eneo la kupigia kura, kutovaa nguo za Chama au picha ya Mgombea, kuwa na maadili mema kazini, Kusimamia zoezi la kuhesabu kura, Kusindikiza masanduku ya kupigia kura kwenda kwenye vituo vya kuhesabia kura,Kuhakikisha usalama wa vituo, usalama wa wagombea pamoja na kusimamia ulinzi na usalama wa wasimamizi wa Uchaguzi wakati na baada ya kutangaza matokeo huku akiwakumbusha muda wa mwisho Kupiga Kura ni saa 10.00 Alasiri ukifika muda huo akae nyuma ya mpiga kura wa mwisho na asiwepo wakufuata.
Kwa upande wake Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi Jimbo la Chato Kaskazini Ndg.Philip George alisema kuwa mpangilio wa kituo cha kupigia kura kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi Mkuu Namba 01 ya 2024,pamoja na kanuni za Uchaguzi Mkuu 2025,Askari anayesimamia uchaguzi anaweza kupiga kura popote atakapo kuwa anasimamia zoezi hilo tofauti na alipojiandikishia ikiwa ametembea na kitambulisho chake cha mpiga kura.
Ndg.George aliongeza kuwa katika zoezi hilo wazee, wajawazito na walemavu wapewe kipaumbelej
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.