Baraza la madiwani limeipongeza Bodi ya Shule na Uongozi wa Shule ya Sekondari Makurugusi kwa usimamizi uliotukuka wa mradi wa ujenzi wa miondombinu ya kidato cha tano na sita kwa fedha za serikali mwaka 2023/2024.Akiongoza kikao cha Baraza madiwani Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa George Magezi amewapongeza uongozi wa shule ya Makurugusi kwa kusimamia vizuri matumizi ya fedha na kuhakikisha mradi umekamilika kwa viwango Bora.
Akitoa Ushuhuda wa namna wamefanikiwa kusimamia mradi Mwalimu mkuu Hashimu Mussa Mushumbushi wa Shule ya Sekondari Makurugusi amesema walitanguliza hofu ya Mungu,wajumbe wote walishirikiana kusimamia ujenzi,na waliweka ulinzi madhubuti wa vifaa vya ujenzi.Pamoja na kukumbana na changamoto ya miondombinu ya usafirishaji wa vifaa Mwalimu Hashimu anasema walihakikisha wanatumia hadi trekta ili vifaa vifike kwa wakati na ujenzi usisimame.
“Namshukuru sana Mungu kwa kutusaidia kufanikisha mradi huu,nawashukuru bodi ya shule na wajumbe wote kwa kuhakikisha kwa pamoja tunafanya kazi nzuri itakayonufaisha vizazi vingi.Zawadi na cheti hiki tulichopata itakua ukumbusho hadi vizazi vijavyo” Mwalimu Hashimu.
Mkurugenzi mtendaji Ndugu Mandia Kihiyo akiwakabidhi zawadi ya Shilingi 300,000 na Cheti cha pongezi amesema Ni vizuri kila mtumishi wa umma akafanya kazi kwa weledi na kuhakikisha fedha za serikali zinatumika kwa usahihi.Shule ya Sekondari Makurugusi walipewa Shillingi 919,425,000.00 kwa ajili ya upanuzi wa kidato cha tano na sita.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.