Barozi wa zao la Pamba nchini Ndg. Agrey Mwanri amewasimika wawezeshaji wa kilimo cha zao la Pamba kutoka kata zote 23 za Chato katika kikao kilichofanyika 9 Nov 2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato.
Akiwasimika wawezeshaji hao Ndg. Agrey amewasisitiza wataalamu hao kutoka sekta za kilimo kutoka kata zotr katika Halmashauri ya Chato amewataka kuzingatia taratibu na kanuni za ulimaji bora wa zao la Pamba nchini.
Aidha Ndg. Mwanri ametoa mafunzo ya umwagilaji wa sumu ya kuuwa wadudu wanao shambulia zao hilo huku
akisisitiza wasimamizi wa vyama AMCOS kuwalipa sitahiki zao wakulima kwa wakati ili kutowakatisha tamaa wakulima wa zao hilo la kibiashara.
Wakati huo huo Mkuu wa wilaya ya Chato Mhe.Deusdedith Katwale amewataka viongozi wa AMCOS pamoja na watendaji kuhakikisha fedha zinazodaiwa na wakulima zinalipwa mara moja vile vile ametoa rai kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Chato Ndg. Mandia Kihiyo kuhakikisha Maafisa Ugani wanakuwa karibu na wakulima ili kuhakikisha katika msimu huu wa mvua ili wakulima wanapate fursa ya kupata ushauri wa kutosha katika msimu huu wa mvua.
Pia amewaagiza madiwani na watendaji wa kata kuhamasisha kila familia ilime walau hekari moja ya zao la biashara ili kukuza uchumi wa wilaya ya Chato.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji akiongea na washiriki wa mkutanoa huo amewaahidi kufanya kazi bega kwa bega na viongozi wa AMCOS huku akisisitiza uadilifu na uwajibikaji kwa kila mtaalamu ndani ya kata ili sote kwa umoja wetu tuwasaidie wakulima wetu katika Halmashauri ya Chato
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.