CHATO KUFUNGUA SHULE 13 MPYA ZA SEKONDARI IFIKAPO JANUARI 2022
Halmashauri ya Wilaya ya Chato iko mbioni kufungua shule 13 mpya za sekondari ifikapo mwezi Januari 2022.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilayana ya Chato Mandia Kihiyo amezitaja shule hizo kuwa ni pamoja na sekondari ya bweni ya wasichana Mbuye iliyopo kata ya Bwina pamoja na Sekondari ya bweni ya wavulana ya Rubambangwe iliyopo kata ya Muungano.
Shule zingine mpya ambazo ziko mbioni kufunguliwa ni pamoja na sekondari ya Nyisanzi na Bukamila zilizopo kata ya Kigongo, Makurugusi na Kibumba zilizoko kata ya Makurugusi, sekondari ya Kanyindo kata ya Nyarutembo, Kanyama kata ya Ilemela, Dkt Kalemani kata ya Bwongera, Muganza kata ya Muganza, Nyambiti kata ya Nyamirembe, Kachwamba, na Itale kata ya Muungano
Kwa sasa Halmashauri kupitia idara ya elimu sekondari inakamilisha mchakato wa usajili wa shule hizo ikiwemo ukaguzi wa uwepo wa mahitaji muhimu na baadae kukamilisha usajili wa shule hizo.
Kukamilika kwa shule hizo kutaifanya Wilaya ya Chato kufikisha shule za sekondari 50 zikiwemo shule 5 za binafsi.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.