• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Malalamiko |
    • Staff Mail |
Chato District Council
Chato District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofis ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chato

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Kilimo
      • Eduction
        • Primary
        • Secondary
      • Fedha
      • Mifugo
      • Maendeleo ya Jamii
      • Water
      • Works
      • Afya
      • Ardhi, na Maliasili
    • Vitengo
      • Procurement
      • ICT
      • Internal Audit
      • Legal
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Uchimbaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Vivutio Vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Health Service
    • Education Service
    • Water Service
    • Agriculture Activities
    • Livestock Activities
    • Fisheries Activities
  • Councilors
    • Councilors List
    • Standing Committee
      • Finance, Planning & Administration
      • Education, Health & Water
      • Environment, Works & Economic
      • HIV/AIDS Control
      • Ethics
    • Schedule
      • Councilors Meting Schedule
      • Meet with Councilor
  • Miradi
    • Planned Projects
    • Miradi inayoendelea Kutekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Repoti
    • By Law
    • Fomu
    • Strategic Plan
    • Huduma ya Mkataba kwa Mteja
    • News Paper
  • Kituo vya Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Matukio
      • Habari

CHATO NDOTO YENU ITATIMIA- RC GEITA

Posted on: June 28th, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Senyamule amesema kutokana na fursa nyingi zilizopo wilayani Chato  na miradi mingi mizuri inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya awamu ya sita mara tu baada ya  kukamilika kwa miradi hiyo itatimiza malengo ya wakazi wa Chato na watanzania kwa ujumla.


Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo leo kwenye kikao maalumu cha baraza la madiwani cha kujadili hoja za Mdhibiti

na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) za mwaka 2020/2021 kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri.


Mkuu wa Mkoa amesema kutokana na Wilaya ya Chato kuwa na uwanja wa ndege, wageni wengi watafika wilayani hapa kwa ajili ya uwekezaji kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ile ya utalii, huduma za Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Chato, mnada wa Ng'ombe wa Buzirayombo na miradi mingine mikubwa iliyopo hapa, hivyo amewaasa  wananchi kuendelea kutoa ushiriakiano kwa serikali ili kuweza kufikia malengo pamoja na kukamilisha miradi hiyo na mingine mipya.


"Najua Wilaya ya Chato inazo ndoto kubwa na nyingi sana, kiasi chake zimeanza kutimia, ndoto kubwa ni kuwa wilaya ya utalii na niwahakikishie ndoto hizo zitatimia" amesema Mkuu wa Mkoa wa Geita.


Kwa upande wa hoja za CAG Mkuu wa Mkoa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chato kuendelea kupata hati safi kwa muda miaka sita mfululizo ambapo ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Chato kuhakikisha hoja zote za CAG zinajibiwa na kufutwa kwa wakati.


"zipo hoja zinazofutwa na  Halmashauri, zinazofutwa ngazi ya Mkoa, na zingine kupitia kwa waziri, kaeni vikao mfute hoja hizi" alisisitiza Mkuu wa Mkoa wa Geita.


Kwa upande wake Mkaguzi mkuu wa nje wa Mkoa wa Geita ACPA Richson Ringo ameshauri Halmashauri kuwajengea uwezo wahasibu, maafisa manunuzi na wale wote wanaohusika na uandaaji wa taarifa za fedha ili waweze kupatiwa mafunzo maalumu na ya kina ili kuepukana hoja za ukaguzi.


Mkuu wa Wilaya ya Chato  mhe. Martha Mkupasi amesema pamoja na Wilaya ya Chato kuwa na miradi ni vyema kuimaraisha usimamizi wa miradi hiyo kwa umakini mkubwa hasa kupitia kitengo cha Manunuzi kwani hoja nyingi zinasababishwa na   watumishi wenyewe. Amewaomba watumishi wa Halmashauri kusimamia kwa umakini ili kuweza kuzuia hoja mpya pamoja na kufunga hoja zilizopo.


Makamu Mwenyekiti wa Halamshauri Mhe. Fortunatus Jangole amesema Halmashauri itachukua hatua kwa wale wote waliosababisha hoja hizo ambapo amesema ni wakati sasa wataalamu wa Halmashauri kuhakikisha inafuta hoja ambazo zinawezekana kufutwa ili kupunguza idadi ya hoja za CAG.

Matangazo

  • MATOKEO YA UDEREVA CHATO DC September 27, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI CHATO DC September 20, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI CHATO May 24, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI CHATO July 19, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • DC BURA AKABIDHI PIKIPIKI 8 KWA MAAFISA MIFUGO

    June 24, 2025
  • CMT YATEMBELEA MIRADI YA BILIONI 1.9

    May 29, 2025
  • NENDENI MKATANGAZE MIRADI NA SHUGHULI ZINAZOFANYWA SERIKALI, MHE. MCHENGELWA

    May 23, 2025
  • MAKAMPUNI 12 KUNUNUA ZAO LA PAMBA CHATO

    May 15, 2025
  • View All

Video

MHE. NDEJEMBI AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUWA NA NIDHAMU NA KUTIMIZA WAJIBU KWA WELEDI
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HOTUBA YA BAJETI TAMISEMI 2019
  • Mwongozo wa Matumizi Bora na Salama wa Vifaa vya TEHAMA
  • MWONGOZO WA KUSIMAMIA NA KUENDESHA TOVUTI ZA SERIKALI
  • MWONGOZO WA OPRAS
  • TAARIFA KWA UMMA UFUNGUZI WA JENGO JIPYA JIPYA CRDB

Tovuti Linganifu

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais- TAMISEMI
  • eMrejesho - Malalamiko/taarifa yeyote kutoka kwa wananchi,Watumishi wa Umma/Wastaafu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Ofisi ya Rais- Utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI

    Postal Address: 116 CHATO

    Telephone: +255282228007

    Mobile:

    Barua pepe: ded@chatodc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Privacy Policy
    • Kanusho
    • Malalamiko
    • map
    • Service

Copyright©2016 CDC . All rights reserved.