Uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chato imeipongeza shule ya sekondari ya ufundi Chato kwa kazi nzuri ya Usimamizi wa miradi ya ujenzi wa madarasa kwenye baadhi ya shule za sekondari.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo,Mandia Kihiyo,mbele ya Baraza la madiwani huku akidai uwepo wa shule hiyo ya ufundi Chato (Chato Technical secondary School) imekuwa msaada mkubwa kwa usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Kutokana na hali hiyo,Baraza la madiwani hao pia limelazimika kutoa cheti cha pongezi pamoja na kiasi cha shilingi 300,000 kwa kamati nzima ya Usimamizi wa mradi wa sekondari ya Kitela ambayo imekamilika kwa aslimia 100.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Christian Manunga,amesema pongezi hizo zinapaswa kuwa chachu kwaajili ya kamati zingine za Usimamizi wa miradi ya jamii ili kuhakikisha fedha inayotolewa na serikali inaendana na ubora wa miradi.
Diwani wa kata ya Chato,Mange Ludomya,ameishukuru halmashauri hiyo kutambua mchango wa shule ya ufundi ya sekondari Chato,na kwamba huo ni mwanga mpya katika usimamizi wa miradi mingine ya maendeleo kwa jamii.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.