Katika kuungana na Dunia kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama , wilaya ya Chato imefikia kilele Cha maadhimisho hayo Leo August 7, 2025 katika kijiji Cha Mlumba.
Wataalamu mbali mbali wa afya kutoka wilayani ikiwa ni pamoja na Afisa lishe wa wilaya Ndg. Isack wametoa Elimu kwa Wananchi juu ya namna gani wanapaswa kunyonyesha watoto pamoja na kuzingatia usafi wakati wa kunyonyesha huku wakiwasihi wanawake kuhakikisha wananyonyesha watoto kwa miaka miwili kabla ya kuwaachisha.
Kwa upande wao wananchi wameushukuru uongozi wa wilaya kwa kupeleka kilele Cha maadhimisho hayo katika kijiji chao kwani wameweza kujifunza masuala mengi yahususiyo unyonyeshaji.
Hata hivyo kila mwaka Dunia huadhimisha wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama,na mwaka huu maadhimisho hayo yalikuwa na kauli mbiu isemayo:
"Thamini Unyonyeshaji; weka mazingira wezeshi kwa mama na mtoto"
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.