Wilaya ya Chato imeanza kutoa chanjo dhidi ya Saratani ya Mlango wa kizazi ambapo kwa kuanzia jumla ya wasichana 5339 watapatiwa chanjo hii.
Chanjo hii ambayo ni endelevu imetolewa na wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto ambayo pia imethibitishwa na shirika la afya Duniani itatolewa kwa wasichana wote wenye umri wa kuanzia miaka 14 kwa lengo la kupambana na Saratani ya Mlango wa Kizazi.
Akizindua Chanjo hiyo katika hospitali ya Wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Shaaban Ntarambe amesema ni wakati sasa mabinti kujitambua na kuacha kufanya mapenzi wakati wa umri mdogo kwani ndio kisababishi kikubwa cha saratani ya Mlango wa kizazi, “ someni kwanza mapenzi mtayakuta tu mkimaliza masomo yenu, msidanganywe na wanaume” Mkuu wa Wilaya aliwaasa wanafunzi waliokuwepo kwenye hafla ya uzinduzi huo.
Mapema aakitoa taarifa ya uzinduzi wa Chanjo, mratibu wa Chanjo bwana Melkizedeck Kimario amesema saratani ya mlango wa kizazi huambukizwa kwa njia ya ngono kutoka kwa mtu mwenye virusi vijulikanavyo kwa jina la Human Papilloma Virus (HPV) ambapo amesema wasichana wenye umri mdogo wako kwenye hatari kubwa ya kupata maabukizi ya HPV.
Chanjo zingine zinazotolewa Wilayani hapa ni ya Kuzuia kifua kikuu, chanjo ya kuzuia kupooza, chanjo ya kuzuia dondakoo, kifaduro pepopunda ,homa ya ini na uti wa mgongo, Chanjo ya kuzuia kichomo, Chanjo ya kuzuia kuharisha, Chanjo ya kuzuia Surua Rubella, na Chanjo ya kuzuia tetanasi.
Aidha chanjo ya kuzuia kupooza itakayotolewa kwa njia ya sindano itatolewa kwa watoto chini ya mwaka 1 na tayari chanjo zimeshapokelewa kiasi cha dozi 4100 na kusambazwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ambapo jumla ya watoto 17,202 wanatarajia kupata chanjo hii kwa mwaka 2018.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.