Mapema hii leo Kamati ya Amani imeungana na Wananchi wa Chato kufanya Maombo Maalumu kwa ajiri ya kuliombea Taifa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 Lengo likiwa ni kuhakikisha Amani inatamaraki tunapoelekea kufanya Uchaguzi Mkuu wa kuwachagua Wabunge, Madiwani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Ibada hiyo imeongonzwa na viongozi mbalimbali kutoka madhehebu ya Adventist Wasabato, jumuia ya Waislamu (BAKWATA), Jumuia ya Wakristu.
Katika Ibada hivyo viongozi wa dini wameitaka jamii kuolinda Amani na kutoruhusu uvunjifu wa Amani kwa namna yoyote Ile bali, kila mmoja afanye maombi ya dhati na kumkabidhi Mwenyezi Mungu kwani yeye ni alfa na omega na ndiye mleta faraja ya kweli penye huzuni na si kujichukulia hatua mkononi.Aidha viongozi hao wa dini wamewataka viongozi wanakwenda kuchagulia kujitahidi kuzingatia haki na usawa katika kuwatumikia Wananchi kwani haki ikikosekana Amani tuliyoilunda kwa Miaka mingi inaweza kutoweka.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.