Katika juhudi za kuimarisha uchumi na kuhifadhi mazingira, Mkuu wa Wilaya ya Chato, Ndg. Louis Bura, aliongoza msafara wa Baraza la Madiwani pamoja na wataalamu mbalimbali kutembelea Msitu wa Shamba la Miti Sao Hill linalopatikana katika Halmashauri ya Wilaya ya Mfindi, Iringa.
Katika ziara hiyo, iliyofanyika tarehe 11Januari, 2025 viongozi hao walipata fursa ya kujifunza zaidi kuhusu umuhimu wa msitu katika kuhifadhi bioanuwai, usimamizi wa rasilimali za misitu, pamoja na fursa za kiuchumi zinazoweza kupatikana kupitia utalii wa mazingira.
Aidha timu ya Wahe. Madiwani pamoja na wataalamu wamepata fursa ya kuonana na Mhifadhi Mkuu wa Misitu Kamishina Silayo ambapo akitoa neno ka ukaribisho ofsini kwa Mkuu wa wilaya ya Mufindi Dkt Linda amesema katika Mwaka ujao wa fedha Serikali imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mazao ya Nyuki na asali wilayani Chato.
Pia, waliweza kujionea mvuto wa mandhari na aina mbali mbali za mimea
Mhe. Louis Bura aliwasisitizia wajumbe wa kikao kwamba ni muhimu kwa jamii kuzingatia umuhimu wa uhifadhi wa mazingira ili kuhakikisha kuwa rasilimali hizi zinabaki kuwa endelevu kwa vizazi vijavyo.
Aidha, aliwataka madiwani na wataalamu kufanya kazi kwa pamoja katika kuboresha uhifadhi wa mazingira katika Wilaya ya Chato, kwa kuanzisha miradi ambayo itasaidia kuendeleza mazingira na kuongeza kipato kwa jamii.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.