Halmashauri ya Wilaya ya Chato, imeshika nafasi ya pili Kitaifa kwa kutoa mfugaji hodari wa Ng'ombe wa maziwa, huku mshindi wa kwanza akiwa ni Ebenezer Nkoh akitokea Dodoma jiji kijiji cha Nzuguni. kufuatia Mashindano ya Maonesho ya nane nane yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma Agosti 8, 2025.
Kinara huyo aliyeitwalia heshima kubwa wilaya yake anafahamika kwa jina la Emmanuel Kabakeza Kalekezi kutoka kijiji cha Butengo, Kata ya Butengorumasa wilayani humo wakati kikundi cha HAMU GRUP kinachojishughulisha na Ujasiliamali na usindikaji kilichopo kata ya Buseresere kikishika nafasi ya tatu kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa Magharibi na kujitwalia Cheti cha ushindi na zawadi ya Tshs. 200,000/= aliyokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mohamed Mtanda aliyekuwa Mgeni rasmi wakati wa kufunga sherehe za kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya nanenane zilizofanyika viwanja vya Nyamhongolo Mnispaa ya Ilemela Jijini Mwanza kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa Magharibi 2025.
Pamoja na Cheti Cha ushindi pia Ndg Kabakeza amepata zawadi ya fedha Taslimu kiasi cha Tshs. 8,000,000/= (Milioni nane tu) ambapo zawadi hizo amekabidhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika Mkoani Dodoma Kitaifa.
Kwa upande wake Ndg Kabakeza amesema kuwa ushindi alioupata ni matokeo ya juhudi za pamoja kati yake na timu ya wataalamu kutoka Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kumpa ushauri wa namna ya kutengeneza malisho bora lakini pia ushauri wa kitabibu kwa mifugo jambo ambalo wataalamu wa Divisheni husika walilifanya bila kuchoka hivyo ushindi huo si wake peke yake bali ni wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kuupata.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg Mandia Kihiyo ameipongeza Serikali kwa mchakato wa kutafuta mshindi na kupatikana Chato lakini pia zawadi ya fedha itakayomsaidia Ndg Kabakeza kuboresha zaidi ufugaji wake huku akimpongeza Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Ndg. Geriad Mgoba kwani imejidhihirisha kuwa yupo vizuri na timu yake ya wataalamu kutoa ushauri wa kitaalamu na kufuatilia utekelezaji wake kwani mwaka 2023/2024 pia alipatikana Mkulima hodari wa zao la Pamba Kitaifa.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.