Mganga mkuu wa Wilaya ya Chato Dr Aristedes Raphael w kampeni ya kuibua wagonjwa wa kifua kikuu. Kampeni hii itahusisha wataalamu wa Afya kuwafuata wananchi mahali waliko ili kuwafanyia vipimo na kutoa matibabu kwa watakaogundilika kua na ugonjwa huo.
Akitoa salamu za ufunguzi wa kampeni hiyo yenye kauli mbiu *“Kifua kikuu kinatibika na kupona kabisa, hata kama una magonjwa mengine”* Dr Aristedes amesema lengo ni kuhakikisha kila mwananchi wa Wilaya ya Chato asiwe na Ugonjwa wa Kifua kikuu. “Tunapiga vita ugonjwa wa kifua kikuu kwasababu unatibika na kupona kabisa,tunaishukuru serikali kupitia Wizara ya Afya imekuja na kampeni ya wiki mbili ili kuongeza uelewa juu ya dalili na utayari wa kufikia vituo vya afya kupata matibabu”.
Akiongea na wananchi waliofika katika uzinduzi wa kampeni hiyo katika Hospitali ya Wilaya ya Chato, Mratibu wa kifua kikuu na Ukoma Dr Mollel amesema matibabu ya kifua kikuu ni bure kuanzia uchunguzi wa awali hadi matibabu,hivyo wamelenga kuyafikia makundi maalumu yanayoshindwa kufika vituo vya afya kwasababu ya mazingira ya kazi zao.“Tunaenda kuwafikia makundi yote maalumu,tutaenda hadi kwenye machimbo kuwafanyia uchunguzi wachimbaji”.
Afisa wa Kifua kikuu na Ukimwi wa wilaya, Mtabibu Michael Ng’wetelwa akitoa elimu kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu amesema ni Ugonjwa sugu unaoambukizwa kwa njia ya hewa,hivyo wananchi wawe makini mara wanapopata dalili wafike vituo vya afya ili kufanya vipimo na kupewa matibabu na sio kununua dawa bila kufanya uchunguzi.
“Ugonjwa sugu ni ule unaokaa kwa mwanadamu zaidi ya siku 14 na kuendelea!Kifua kikuu kinadhibitiwa kwa chanjo” Mtabibu Michael Ng’wetelwa.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.