Serikali Wilayani Chato imezindua rasmi zoezi la utoaji wa huduma ya Chakula kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari.
Zoezi hilo limezinduliwa kwenye kilele cha juma la elimu kilichofanyika kiwilaya kata ya Mganza na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu waliopo wilayani hapa.
Katika hotuba yake Mkuu wa Wilaya ya Chato aliyewakilishwa na Katibu Tawala wa Wilaya ndugu Elias Makori amesema utoaji wa Chakula shuleni utaongeza mahudhurio kwa wanafunzi wengi sambamba na kupanda kwa kiwango cha ufaulu kwa Wilaya ya Chato.
“huo ni wajibu wetu sisi wazazi kuhakikisha tunachangia chakula angalau wapate uji na pale kuna pokuwa na uwezo wapate makande ” alisema Mkuu wa Wilaya.
Naye diwani wa kata ya Mganza mhe. Mwita Tagota amesema ni wajibu wa wazazi kuhakikisha watoto wao wanapata huduma ya chakula wawapo shuleni kwa kutoa sehemu ya chakula ambacho wazazi wamekuwa wakiwapa wanafunzi wawapo nyumbani na kupelekwa shuleni bila kuathiri uchumi wa familia.
Katika risala yao wanafunzi wameomba serikali kuanzisha shule sitiri ili kupunguza umbali mrefu wa wanafunzi kwenda shule. Wanafunzi hao wamesema mpango wa utoaji wa chakula shuleni ni msingi mzuri wa ukuaji wa stadi za kujua kusoma, kuhesabu na kuhandika hivyo wameiomba jamii kulipa kipaumbele suala hilo.
Juma la elimu limeenda sambamba na maonesho ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi katika ujifunzaji wa kila siku na utoaji wa tuzo kwa shule na walimu waliofanya vizuri katika sekta ya elimu kwa mwaka 2017/2018.
Kaulimbiu yamaadhimishio hayo ni Stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu KKK ni msingi wa kuelekea uchumi wa viwanda.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.