Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri ameagiza kaya zisizokuwa na vyoo wilayani hapa kuhakikisha wanachimba vyoo hadi kufikia tarehe 30 Julai 2019 kaya hizo ziwe na vyoo.
Mkuu wa Wilaya ametoa agizo hilo wakati wa hitimisho la Kampeni ya kitaifa ya Nyumba ni Choo Wilayani Chato iliyofanyika stendi ya Muungano inayoratibiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI chini ya balozi wa kampeni hiyo msanii Mrisho Mpoto.
Mkuu wa Wilaya amesema kwa takwimu zilizopo kaya 1,155 kukosa vyoo bora katika Wilaya ya Chato si suala la kuvumilia na hivyo kuagiza wananchi wote wajenge vyoo na ambavyo havijaboreshwa kuhakikisha vinafanyiwa maboresho hadi kufikia muda huo kila kaya hizo ziwe na vyoo.
“Mwisho wa mwezi wa saba kwa ambaye hatakuwa hana choo akamatwe, apigwe faini ya shilingi elfu 50,000 kisha atuoneshe sehemu anayojisaidia” alisisitiza Mkuu wa Wilaya.
Aidha Mkuu wa Wilaya ameagiza kuanzia tarehe 17 Juni 2019 maafisa afya waanze msako nyumba hadi nyumba kukagua usafi katika maeneo yanayozunguka nyumba ambapo ameagiza kwa nyumba ambazo zitakutwa zimezungukwa na uchafu nazo zipigwe faini.
Akisoma taarifa ya Wilaya kuhusu Usafi wa Mazingira afisa afya bwana George Luhumbika amesema hadi kufikia mwezi Machi 2019 jumla ya kaya 61,941 za Chato zilizoingizwa kwenye mfumo wa usafi na mazingira wa kitaifa, kaya 60790 zina vyoo sawa na 98.1% na kaya 1155 hazina vyoo sawa na 1.86%.
Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba ni Choo Msanii Mrisho Mpoto amesema ni aibu kwa watanzania kuendelea kufundishwa namna ya kunawa mikono au kutokuwa na choo, ambapo amesema choo bora hakihitaji gharama kubwa kama mtu ataamua katika familia yake.
“Mheshimiwa DC mimi nitasikitika nikisikia kuwa hadi leo hii watu hawajui kunawa mikono…, Choo bora hakiitaji gharama kubwa, choo bora kinatakiwa kiwe na mfuniko, kisakafiwe na kiwe na bomba la kutolea hewa chafu, choo bora kiwe na maji na sabuni. Alisisitiza Mrisho Mpoto.
Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri akiongoza maandamano ya kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba ni Choo katika kata ya Muungano
Mkuu wa Wilaya akiwa na viongozi wengine wakiwa wamesimama kwenye Bendera aliyoipandisha kwa 57% ambayo ni asilimia ya kaya zenye vyoo viliyoboreshwa katika Wilaya ya Chato huku kukiwa na kazi ya kufikia kaya zote ifikapo Julai 30 2019.
Balozi wa Usichukulie Poa Nyumba ni Choo Mrisho Mpoto akiongea na wananchi wa wa kata ya Muungano kuhusu matumizi ya Vyoo na unawaji wa mikono
Sehemu ya meza kuu wakipunga mkono kuashiria kupokea kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba ni Choo
Wasanii wakitoa burudani wakati wa kampeni hiyo iliyofanyika stendi ya Muungano
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.