Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani Mkuu wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri akipima virusi vya UKIMWI kwenye maadhimisho yaliyofanyika Kimkoa wilayani Chato kata ya Bwanga. Mkuu wa Wilaya ya Chato alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita
Mkuu wa wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri akichukuliwa vipimo kabla ya kuchangia damu kwenye maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika Wilayani Chato kata ya Bwanga
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Eliurd Mwaiteleke akipima virusi vya UKIMWI kwenye maadhimisho ya siku UKIMWI yaliyofanyika Kimkoa wilayani Chato kata ya Bwanga
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashari ya Wilaya ya Chato akichukuliwa vipimo kabla ya kuchangia damu kwenye maadhimisho hayo
Mkuu wa idara ya Utumishi na Utawala Halmashauri ya Wilaya ya Chato Calolina Kayombo akifurahia jambo mara baada ya kupima virusi vya UKIMIWI katika maadhimisho hayo
Askari wa Usalama barabarani wa Wilayani Chato nao pia walijitokeza kupima virusi vya UKIMWI
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye foleni kwa ajili ya kipima Virusi vya UKIMWI katika maadhimisho hayo
Diwani wa kata ya Bwanga (kulia) Nuhu Mahamud akichangia damu, kushoto kwake ni katibu wa wazazi wilaya ya Chato Ally akipande naye akijiandaa kuchangia damu
Mkuu wa Wilaya ya Chato akihutubia mamia ya wananchi (hawapo pichani) ambapo amewasisitiza kupima virusi vya UKIMWI mara kwa mara na pia kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa mbalimbali
Baadhi ya wananchi waliofika kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika kimkoa Wilayani Chato kata ya Bwanga
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.