Mkuu wa Wilaya Mh. Louis Bura leo tarehe 30.9.2025 amefungua Zahanati ya Nyarututu iliyopo Kata ya Bwanga. Zahanati hii imeanza rasmi kazi leo ,Ujenzi ukiwa umegharimu jumla ya Tsh 92,410,714.29 fedha kutoka Serikali kuu (TASAF) na Tsh 7,700,000.00 nguvu za wananchi na inatarajiwa kuhudumia zaidi ya wakazi 65,000 wa kijiji cha Nyarututu na maeneo ya Jirani.
Akizungumza na wananchi waliohudhuria hafla ya Ufunguzi, Mh. Bura amewashukuru na kuwapongeza wananchi kwa Ushirikiano mkubwa walioutoa tangu Ujenzi ulipoanza hadi kukamilika.
“Niwapongeze sana kwa umoja wenu na ushirikiano mliotoa kwa uongozi wa kijiji na serikali katika kuhakikisha Zahanati hii inakamilika na kuanza kutoa Huduma! Niwaombe sasa mtunze vizuri zahanati hii, mali zilizopo ndani ya zahanati na zaidi sana Watumishi walioletwa kuwahudumia!tuache tabia ya kuwakataa watumishi,Tuwape ushirikiano wa kutosha ili tupate huduma bora na kwa wakati.”
Aidha Mkuu wa wilaya amewashukuru wananchi kwa kufika kwa wingi kwa ajili ya ufunguzi wa Zahanati na kuwakumbusha juu ya kushiriki Uchaguzi na kupiga kura tarehe 29.10.2025 kwa wingi huo huo.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.