Mkuu wa Wilaya ya Chato mhandisi Mtemi Msafiri Semeon ameagiza mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Eliurd Mwaiteleke kutokumwongeza muda mkandarasi wa mradi wa maji wa Imalabupina Ichwankima kutokana na kusuasua kwa utekelezaji wa chujio la maji linalojengwa Nyamirembe na utandazaji wa mambomba ya maji.
Mkuu wa Wilaya ametoa agizo hilo leo wakati akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani hapa ziara ilihudhuriwa pia na waziri wa Nishati mhe.Dkt. Medard Kaleman na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato.
“hajatoa sababu yoyote ya msingi ya serikali kumwongeza muda na kama ni hela alishalipwa… sisi ikifika tarehe tunaanza kumakata hela, kuna vifaa havipo site, sisi tunataka water treatment ikalimilike wananchi waanze kupata huduma ya maji” alisistiza Mkuu wa Wilaya.
Naye mhe. Dkt. Kalemani amesema pamoja na kumweleza mkandarasi huyo kukamilisha mradi huo kwa wakati lakini bado kazi ya mkandarasi huyo bado hairidhishi na hivyo amemwagiza kuongeza vifaa eneo la kazi pamoja na kuongeza muda wa kufanya kazi na idadi ya mafundi na vibarua ili kazi ikalimilike ndani ya muda uliopangwa.
Mradi wa maji wa Imalabupina Ichwankima wenye thamani ya Shilingi bilioni 8.2 unatekelezwa na wakandarasi Ndeenengo Senguo Co. LTD. na MM industry Co. LTD kwa mkataba wa miezi 12 ulianza mwezi Mei mwaka 2017 na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba 2018.
Miradi mingine iliyotembelewa na viongozi hao ni pamoja na ujenzi wa Bandari ya Nyamirembe, Soko la Kimataifa la Kasenda, Shule ya sekondari ya Zakia Meghji na kituo cha Afya cha Kachwamba ambapo Mkuu wa Wilaya ameagiza kufanyika marekebesho kwenye ujenzi wa njia ya watembea kwa miguu (walkway) kituoni hapo na kuondoa baadhi ya milango iliyo chini ya kiwango
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.