Mkuu wa wilaya ya Chato Mhe. Mhandisi Deusdedith J. Katwale, leo Novemba 9, 2023 amefanya kikao na Waganga Wafawidhi kutoka katika Zahanati na Vituo vya Afya pamoja na Hospital ya Kanda Chato.
Kikao hicho kilichoketi katika ukumbi wa J's Chato kilikuwa na lengo la kuwajulisha juu ya tamasha kubwa (Chato Utalii Festival) litakaloanza tarehe 26 Novemba 2023 na kutamatika 03 Disemba 2023.
Mhe. Katwale amewafahamisha wataalamu hao kuwa katika Tamasha hilo mtaji wa kwanza ni Afya ya washiriki, hivyo wanapaswa kujikita katika kutoa huduma za afya kwa watalii watakaofika kutoka nje na wanaotoka ndani ya wilaya yetu.
" Nashauri watumishi wa kada zote hususani wataalam wa Afya washiriki kikamilifu upande wa riadha (Marathon) ili kujiweka sawa mwili pamoja na kuburudika kwa kukutana na watu kutoka maeneo mbalimbali na kubadilishana nao mawazo, Nyinyi wataalam wa Afya muhimu sana mjipange kimikakati katika kuhakikisha huduma za Afya zenye kiwango cha ubora zitapatikana kikamilifu muda wote wa Tamasha kama ilivyo kawaida yetu hapa Chato kipaombele chetu ni huduma bora" Alisema Mhandisi Katwale.
Aidha Katwale amehitimisha kwa kuwasisitiza wajumbe wa kikao kuwa mabalozi wa kutangaza suala la " *CHATO UTALII FESTIVAL"* kwani wafanyabiashara watanufaika kwa kutangaza na kuongeza wateja wa biashara zao, Wataelimika kupitia makongamano pia wataburudika kupitia, Mbio za baiskeli, wasanii maarufu kama vile Baba Revo, Mandonga mtu kazi ( Atapigana), Barnabas, Mrisho Mpoto, Beka flavour, Sholo Mwamba, Ibra Mzalendo(Zingibari) na wasanii wengine wakubwa ambao kamati bado inafanya nao mazungumzo kuhakikisha kuwa watakuwepo.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.