• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Malalamiko |
    • Staff Mail |
Chato District Council
Chato District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofis ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chato

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Wilaya
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Kilimo
      • Eduction
        • Primary
        • Secondary
      • Fedha
      • Mifugo
      • Maendeleo ya Jamii
      • Water
      • Works
      • Afya
      • Ardhi, na Maliasili
    • Vitengo
      • Procurement
      • ICT
      • Internal Audit
      • Legal
    • Muundo wa Utawala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Uchimbaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Vivutio Vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Health Service
    • Education Service
    • Water Service
    • Agriculture Activities
    • Livestock Activities
    • Fisheries Activities
  • Councilors
    • Councilors List
    • Standing Committee
      • Finance, Planning & Administration
      • Education, Health & Water
      • Environment, Works & Economic
      • HIV/AIDS Control
      • Ethics
    • Schedule
      • Councilors Meting Schedule
      • Meet with Councilor
  • Miradi
    • Planned Projects
    • Miradi inayoendelea Kutekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Repoti
    • By Law
    • Fomu
    • Strategic Plan
    • Huduma ya Mkataba kwa Mteja
    • News Paper
  • Kituo vya Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Matukio
      • Habari

DC CHATO ATAHADHALISHA WANANCHI DHIDI YA MATAPELI SHAMBA LA MITI SILAYO

Posted on: June 6th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Martha Mkupasi  amewataka wananchi wa kata ya Bwanga wanaopakana na Shamba la miti la Silayo kuwa makini na matapeli  wanaouza ardhi ambayo ni sehemu ya hifadhi pamoja na kuchukua mali za wananchi.


Mkuu wa Wilaya ametoa tahadhali hiyo leo tarehe 06.06.2022 wakati wa mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi wa kijiji cha Nyarututu kata ya Bwanga.


Mkuu wa Wilaya amesema amekuwa akipokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wa maeneo hayo wakidai kutapeliwa na watu ambao wamewauzia ardhi ya hifadhi ya serikali.


"Tuachane kuuza ardhi ya hifadhi si maeneo yenu, ni ya mali ya serikali, kuna watu wengi wamekuja kwangu kulalamika wametapeliwa na wanataka kurudishiwa fedha zao, acheni kununua ardhi ya hifadhi.


Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Chato amesema kuna watu wamekuwa wakivaa sare za mgambo na kujitambulisha kuwa wametumwa na Serikali ambapo wamekuwa wakichukua mali za wananchi ikiwemo mazao, kuku, baiskeli.


Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi hao kuwa makini na watu wa aina hiyo na amewataka wananchi kutoa taarifa haraka kwenye ofisi za serikali.


"wananchi mnadanganywa sana, mtu anafika kwenu anachukua kuku, mazao, basikeli, anasema mimi nimetumwa na serikali, huo ni uongo, shirikianeni na  toeni taarifa za wizi huu" amesisitiza Mkuu wa Wilaya.


Mapema Mkuu wa Wilaya ameeleza mafanikio ya serikali ya awamu ya sita Wilayani ikiwemo ujenzi wa hospitali ya rufaa ya kanda ya Chato ambapo zaidi ya shilingi bilioni 40 zimetolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa ujenzi na vifaa tiba sambamba na Sekta ya elimu ambapo zaidi ya shilingi Bilioni 5 zimeletwa hadi sasa.


Katika Mkutano huo wa kusikiliza kero Mkuu wa Wilaya aliambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri, na taasisi zingine za serikali ikiwemo TARURA,  RUWASA na TANESCO.

Matangazo

  • MATOKEO YA UDEREVA CHATO DC September 27, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI CHATO DC September 20, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI CHATO May 24, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI CHATO July 19, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • DC BURA AKABIDHI PIKIPIKI 8 KWA MAAFISA MIFUGO

    June 24, 2025
  • CMT YATEMBELEA MIRADI YA BILIONI 1.9

    May 29, 2025
  • NENDENI MKATANGAZE MIRADI NA SHUGHULI ZINAZOFANYWA SERIKALI, MHE. MCHENGELWA

    May 23, 2025
  • MAKAMPUNI 12 KUNUNUA ZAO LA PAMBA CHATO

    May 15, 2025
  • View All

Video

MHE. NDEJEMBI AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUWA NA NIDHAMU NA KUTIMIZA WAJIBU KWA WELEDI
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • HOTUBA YA BAJETI TAMISEMI 2019
  • Mwongozo wa Matumizi Bora na Salama wa Vifaa vya TEHAMA
  • MWONGOZO WA KUSIMAMIA NA KUENDESHA TOVUTI ZA SERIKALI
  • MWONGOZO WA OPRAS
  • TAARIFA KWA UMMA UFUNGUZI WA JENGO JIPYA JIPYA CRDB

Tovuti Linganifu

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais- TAMISEMI
  • eMrejesho - Malalamiko/taarifa yeyote kutoka kwa wananchi,Watumishi wa Umma/Wastaafu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Ofisi ya Rais- Utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI

    Postal Address: 116 CHATO

    Telephone: +255282228007

    Mobile:

    Barua pepe: ded@chatodc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Privacy Policy
    • Kanusho
    • Malalamiko
    • map
    • Service

Copyright©2016 CDC . All rights reserved.