Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Martha Mkupasi leo amezindua rasmi Kampeni ya Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 wa Wilaya ya Chato ambapo jumla ya watoto 116,155 wanatarajiwa kupata Chanjo hiyo.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya amewaagiza wazazi na walezi wote wenye watoto kuhakikisha wanatoa ushiriakiano kwa watoa huduma watakaopita majumbani kutoa chanjo na mahali popote palipo andaliwa kuanzia leo jumtano hadi siku ya jumamosi ambapo zoezi hilo litahitimishwa.
Zoezi la uzinduzi wa kampeni ya Chanjo ya Polio limefanyika kijiji cha Msilale kata ya Chato na litaendelea katika maeneo yote ya Wilaya ya Chato na linatarajiwa kuhitimishwa siku ya Jumamosi tarehe 21 Mei 2022.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.