Mkuu wa wilaya ya Chato Mhe
Deusdedith Katwale ameitoa kauli hiyo mapema leo hii katika Kata ya Bwanga ambako zoezi la kufanya usafi wa mazingira kiwilaya limefanyika ikiwa ni Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi kama ambavyo tumejiwekea utaratibu huo kama taifa na sasa ni desturi yetu kama watanzania.
Aidha Mhe. Katwale amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha na kuhakikisha wanafanya usafi katika maeneo yao ameongeza kwa kusema, "haina maana mimi na timu yangu mpaka nitoke Chato kuja kukwambia fanya usafi katika eneo lako wakati wewe mwenyewe unaona hali halisi na kuanzia sasa kila mmoja aone kuwa usafi ni jambo ambalo huwezi kulitenganisha na maisha ya mwanadamu"
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chato Ndg. Mandia Kihiyo amemshukuru Mhe. Mkuu wa wilaya kwa kuwa tayari kuja kushiriki katika usafi pamoja na watumishi wa umma na wananchi wa Bwanga uliofanyika katika Soko la Bwanga ambapo mwitikio umekuwa mkubwa jambo ambalo linaashiria sasa wana Bwanga na Chato kwa ujumla wameamua kufanya kazi kama timu moja.
Pia ameongeza kwa kusema Chato hatuna magonjwa ya milipuko kama ilivyo katika maeneo mengine jambo ambalo ni matunda ya kuweka maeneo yetu kuwa safi kwani usafi ni afya.
Mhe Diwani ya Kata ya Bwanga amemkaribisha Mhe. Mkuu wa wilaya ya katika Kata hiyo huku akimuahidi yeye pamoja na wana Bwanga wapo tayari kumpa ushirikiano mda na wakati wowote atakapohitaji.
Katika hatua nyingine Mhe Diwani amemwomba Mhe. Mkuu wa wilaya kuangalia namna ya kufanya maboresho ya soko la Bwanga kwani limekuwa finyu na kupendekeza kujengewa Soko la Ghorofa.
Akihitimisha zoezi hilo la usafi Mkuu wa wilaya ya Chato Mhe. Deusdedith Katwale amewataka kila mwananchi kutimiza wajibu wake ili sote kwa umoja wetu tuilinde Chato yetu, ameongeza kwa kusema, "haipendezi mwananchi unakaa eneo lako ni chafu lakini unasubiria Mkuu wa wilaya na Timu yake au Mkurugenzi waje wakwambia eneo lako chafu ndo ufanye usafi"
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.