Hayo yamesemwa na Mhe. Mkuu wa wilaya ya Chato Eng. Deusdedith Katwale katika maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa shule ya Sekondari Jikomboe chini ya kauli mbiu isemayo " Imarisha Maadili na Upendo kwa familia Imara" akiongea na viongozi wa Dini na Serikali pamoja na wananchi waliohudhulia katika maadhimisho hayo Mhe. Katwale amesisitiza familia kudumisha amani na upendo kama msingi wa kuwa na jamii yenye maadili.
Ameongeza kwa kusema " bila kuwa na familia imara basi tegemea kuma na jamii tegemezi kwani kila kitu katika jamii zetu kinajengwa na msingi wa familia imara"
Aidha Mhe. Katwale amesisitiza kama tunataka kurejesha misingi ya Maadili basi tunahitaji kufanya mambo makuu manne katika jamii zetu kama familia ambayo; imani thabiti kama msingi wa ndoa, uchumi ndani ya familia, kuwa na elimu pamoja na matumizi sahihi ya teknolojia haya mambo yanapokosekana basi ndipo tunaona jamii zetu zinakuwa na tabia za mmonyoko wa maadili kama vile vitendo vya ushoga, kusagana na ulawiti, mauaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chato Ndg. Mandia Kihiyo ameomba wazazi kama kiunganishi mhimu ndani ya familia kuendelea kuwa msitari wa mbele katika malezi na kuendelea kulinda utu wa jamii zetu na taifa kwa ujumla.
Akitoa neno la shukrani Ndg. John Mgaya amemshukuru Mhe. Mkuu wa wilaya kwaniaba ya wanafamilia wote waliofika katika maadhimisho hayo kwa hotuba nzuri ambayo ameitoa na kumwaidi kwenda kuyaishi maneno aliyowaasa ili jamii zetu ziwe na amani na upendo na kuwa na jamii zenye maadili mazuri.
Akihitimisha maadhimisho hayo Mhe. Mkuu wa wilaya amepata fursa ya kutembelea banda la lishe na kupata fursa ya kupima uzito pamoja na kimo ili kujua uwiano wa uzito wake ambapo amewaasa wananchi kutembelea banda hilo ili kujua afya zao.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.