Ni katika kikao kazi cha kuhamasisha wananchi kujitokeza katika zoezi la Chanjo ya Mifugo dhidi ya Homa ya Mapafu na Kichaa cha Mbwa.
Mhe. Mkuu wa wilaya ya Chato Eng. Deusdedith Katwale ameitoa kauli hiyo alipokuwa katika mkutano uliowakutanisha ma afisa mifugo, wadau wa sekta ya mifugo, wafugaji maarufu, watendaji wa kata na vijiji, wenyeviti wa vijiji na vitongoji pamoja na wananchi wa kata za tarafa ya Kachwamba uliofanyika katika shule ya sekondari Buhigo ukiwa na lengo la kujengeana uelewa juu ya zoezi la chanjo ya Homa ya Mapafu na Kichaa cha Mbwa.
Mhe. Katwale amesema mifugo hawa tunaombizana leo tukawachanje ni kwababu tunataka kulinda afya zetu na jamii inayotuzunguka kwani madhala ya kutochanja mifugo ni ghali sana katika matibabu na pengine kifo mfano Kichaa cha Mbwa.
Aidha Mhe Katwale ameendelea kuwaasa wafugaji pamoja na kuwa tunakwenda kutoa chanjo kwa mifugo amewataka wafugaji pamoja na serikali za vijiji na vitongoji kuanza kuona ni namna gani wanaboresha shughuli za ufugaji ikiwa ni pamoja na kuanza kutenga maeneo kwa ajili ya malisho, kufuga kisasa na kuachana na ufugaji wa mazoea.
Wahe. Madiwani kutoka tarafa ya Kachwamba kwa kauli moja wamewaomba wakulima na wafugaji kuancha tabia ya kufunga mapanda( njia za kupitisha ngombe) kwa lengo la kuondoa migogoro na chuki baina ya pande hizo mhimu katika sekta hii ya Kilimo na Mifugo.
Afisa Mifugo wa wilaya Ndg. Tiba amewataka wafugaji kuhakikisha mifugo yao inapata chanjo kwani gharama ipo chini na rafiki kwa kila mfugaji " mfano chanjo ya Homa ya Mapafu itatolewa kwa ng'ombe shilingi 700 kondoo na mnuzi kwa shilingi 600 lakini kwa chanjo ya Kichaa cha Mbwa itakuwa shilingi 2000"
Aidha Ndg. Tiba amewaomba wananchi wa kata ya Kachwamba kila mmoja kwenda kuwa balozi wa mwenzake katika kuhakikisha kila mmfugo unapata chanjo ili jamii yetu iwe mahala salama pa kuishi na kufanya shughuli za uzalishaji.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.