Halmashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita imetakiwa kuimarisha mbinu na usimamizi wa ukusanyaji mapato ya ndani huku shughuli za kisiasa zikitakiwa kutoathiri zoezi hilo ili kuongeza kiwango cha ukusanyaji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miradi ya maendeleo hususani miradi vipolo iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa wilaya ya Chato Mhe. Said Nkumba katika mkutano wa Baraza la madiwani wa halmashauri hiyo lililoketi machi 20, 2024 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya, likiwa ni la robo ya pili ya mwaka wa fedha 2023/2024.
Mhe. Nkumba amesema wilaya kuwa ya mwisho kwa ukusanyaji mapato ni fedheha na aibu kubwa, hivyo amewataka watumishi hususani wanaokusanya mapato kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali waongeze ufanisi ili kuleta matokeo chanya kwani kila mmoja kwa nafasi yake akitekeleza vizuri majukumu yake ana mchango mkubwa wa kuleta maendeleo ya wilaya yetu na Taifa kwa ujumla.
Aidha Mhe.Nkumba ametoa onyo kali kwa yeyote atakayefanya ubadhilifu wa fedha zinazoelekezwa kwenye miradi, kwani hataangalia ninani aliyehusika bali sheria itafuata mkondo wake, huku akielekeza kuwa miradi yote hata ile inayotoka Serikali kuu wananchi washirikishwe kwani ushiriki wao utawafanya waone miradi hiyo ni yao na hivyo kuimarisha ulinzi.
"Katika wilaya hii mimi ni mgeni, ninawaahidi ushirikiano mkubwa katika kazi. Nidhamu ni kitu cha msingi kuleta mafanikio, nahimiza mahusiano mazuri kazini Chato iwe moja sitaki migawanyiko.Tuwaheshimu viongozi wetu wenye dhamana kwa wananchi Wahe. Wenyeviti, Madiwani, pamoja na Mbunge wetu sitapenda kusikia lugha za kejeli dhidi yao..Namalizia na wanaofugia mjini wanaharibu miundombinu, Afisa mazingira na Afisa mifugo angalieni sheria inasemaje na ifuatwe. Amesema Nkumba"
Naye Mwenyekiti wa Baraza la madiwani Mhe. Batholomeo Manunga amewataka maafisa elimu Msingi na Sekondari kuwasimamia walimu katika ufundishaji wenye tija ili kuinua ufaulu, huku akisisitiza fedha za mfuko wa jimbo ziende kupunguza makali ya michango ya wananchi na si kuwa sadaka za viongozi wachache wabadhilifu hivyo zikafanye kazi iliyokusudiwa.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.