▪︎Ni katika kikao alichoketi
mapema hii leo na
wakuu wa idara pamoja
na vitengo katika ukumbi
wa mikutano ofsini
kwake.
1. Kila Mkuu wa Idara ahakikishe anatimiza wajibu wake kwa uadilifu na ufanisi wenye kuleta matokeo chanya katika eneo analolisimamia
2. Kila mmoja akawe jicho la Serikali katika eneo lake la kazi hasa katika kusimamia fedha za Miradi zinazokwenda kutekeleza miradi mbalimbali ndani ya Halmashauri,
"_Jiepusheni na ubadhilifuwa Fedha na Mali za Serikali"_
3. Kasi ya ukusanyaji wa Mapato iongezeke ikiwa ni sambamba na kuunda timu maalumu ya kufatilia mapato ya ndani ya Halmashauri.
4. Idara ya Utumishi na utawala fanyeni kazi zenu kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni za kiutumishi katika kuwahudumia watumishi wote wa umma bila kujali cheo chake au mahala anapotoka.
NB:
Madai ya uhamisho, posho ya kujikimu, msawazo wa watumishi hasa kada ya elimu ufanyike kwa kuzingatia jinsia lakini nendeni mkasimamie sitahiki zote za watumishi wote.
_"Haipendezi kuona mtumishi flani kahamia juzi unakuta yeye kalipwa stahiki ile ile ambayo kuna mfanyakazi uko nae ana zaidi ya mwaka lakini stahiki yake ile ile bado hajapatiwa"_
5. Viongozi wote kuanzia ngazi ya Kijiji na Kata jengeni utamaduni wa kuwasiliza wananchi mnaowahudumia ikiwa ni pamoja na kutatua kero zao.
6. Watumishi wa Umma fanyeni kazi kama timu, jihadhalini na makundi katika utumishi wa umma.
7. Hakikisheni Miradi yote vipolo inakamilika ikiwa ni sambamba na kulipa Madeni yote ya Wazabuni katika Halmashauri yetu.
8. Ofisi ya Mganga Mkuu wa wilaya wekeni utaratibu wa kuwahudumia wazee wetu katika hospitali zetu na vituo vyetu vya kutolea huduma kama mwongozo wa Serikali unavyotutaka.
9. Idara za Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari simamieni nidhamu, na uwajibikaji wa waalimu katika shule zote ndani ya Halmashauri, " _Nimesikia na kuambiwa mambo mengi yanayoendelea ndani ya idara hizi niwaombe sana, nendeni mkabadirike kwani ninyi mnasimamia kundi kubwa la watumishi ndani ya Halmashauri yetu_ "_
10. Maelekezo ya viongozi toka ngazi ya wilaya, mkoa na kitaifa ni mhimu ni lazima kuheshimika.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.