Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita, mapema hii leo Septemba 15, 2024 amekula kiapo cha kuwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Akimuapisha Mhe. Hakimu Mfawidhi wilaya ya Chato Adv. Amalia Ludovick Mushi amemtaka kuhakikisha anasimamia Sheria na kutenda haki katika mchakato wote wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Jimbo la Chato ikiwa ni sambamba na kuwaasaa Viongozi wote wanaogombea nafasi mbalimbali ndani ya uchaguzi huu kujiepusha na vitendo vya rushwa, chuki na ukabila.
Kiapo hicho kimeshuhudiwa na Viongozi mbalimbali, ambapo kila mmoja aliyeshuhudia kiapo hicho amesikika akisema, "ni imani yake kuwa Uchaguzi huu utakuwa huru na wa haki kwa kila mwananchi
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.