Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato ndugu Mandia Kihiyo leo tarehe 10 Machi 2022, ametimisha rasmi mafunzo ya siku mbili kwa wakusanya taarifa 400 kutoka kata zote za Chato yaliyokuwa yakifanyika katika ukumbi wa chuo cha VETA Chato huku akisisitiza suala la nidhamu wakati wa zoezi hilo.
Mkurugenzi mtendaji amesema ni wazi kuwa vijana hao 400 waliochaguliwa kufanya kazi hiyo wamekidhi vigezo hivyo anatarajia zoezi litafanyika kwa ufanisi na kwa muda mfupi zaidi.
"niwaombe mkafanye kazi hii kwa uadilifu mkubwa, ni wengi waliomba kazi hii lakini ninyi mmeaminiwa zaidi hivyo sitegemei mtuangushe" alisema Mkurugenzi mtendaji.
Katika hatua nyingine mkurugenzi Mtendaji amesisitiza suala la uzalendo kwa vijana hao katika kufanikisha kazi hiyo ambayo itafanyika kuanzia tarehe 14 Machi, 2022 na inatarajiwa kukamilika tarehe 21 Machi, 2022.
Mafunzo hayo yameenda sambamba na kiapo cha uamifu mbele ya hakimu wa mahakama ya Wilaya Chato kwa wakusanyaji wote wa taarifa.
Zoezi la ukusanyaji wa taarifa litafanyika kwa kutumia simu janja ambapo taarifa za makazi zitajazwa katika mfumo huo maalumu ulioandaliwa na serikali ambapo kila makazi yanatakiwa kuwa na namba maalumu ya utambuzi ambayo itabandikwa katika jengo husika sambamba na majina ya mitaa na barabara kama yalivyokubaliwa na uongozi wa serikali za mitaa.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.