Mkuu wa wilaya ya Chato Mhe Deusdedith John Katwale akikabidhi mikopo hiyo katika Ofisi za Halmashauri kwa vikundi amewaasa wanakikundi wote kuwa waadirifu na kufanya kazi kulingana na maandiko waliyoandika wakati wanaomba Mikopo hiyo.
Mhe. Katwale ameongeza kwa kusema ' ndugu zangu wanachi wa Chato Serikali yenu inawapenda na Mhe Rais ana imani kubwa nanyi hivyo onyesheni fadhira kwa kufanya kazi ili sote kwa pamoja tujiletee maendeo'
Katika hatua ingine Mhe Katwale amekabidhi pikipiki sita kwa kikundi Umoja ni Nguvu Kibehe zenye thamani ya tsh Mil 15 kinachotoka katika kata ya Kigongo.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chato Mhe. Christian Manunga amewaomba wananchi pamoja na viongozi katika Halmashauri kumpa ushirikiano Mhe. Mkuu wa wilaya mpya ili aweze kutimiza wajibu wake ambao Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemwamini na kumpatia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chato Bw. Mandia Kihiyo amewaomba wananchi kuchangamkia fursa hiyo kwa kuomba kupitia mfumo wa mikopo ambao ni www.tplmis.go.tz kwani fedha hizo zinatolewa bila riba
Kwa upande wa vikundi vilivyopokea Mikopo hiyo wameahidi kwenda kutumia fedha hizo kulingana na maandiko yao.
Kwa upande wa vijana waliopewa pikipiki hizo wameahidi kuztumia kwa kufuata sheria na kanuni zote za barabarani.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.