Mhe. QS Omary Kipanga ameitoa kauli hiyo mapema hii Julai 05, 2024leo alipokuwa katika ziara ya kikazi katika Halmashauri ya wilaya ya Chato ambapo alipata fursa ya kutembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa Shule Maalumu ya Mbuye inayojengwa na shirika la nyumba la taifa (NHC) ambayo mpaka kukamilika kwake itagharimu kiasi cha billion 4.7
Akizungumza na viongozi wa chama na Serikali waliokuwa wameambatane nae katika ziara hiyo Mhe. QS Omary Kipanga amewataka Shirika la Nyumba la Taifa kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati kama ulivyokusudiwa kwani fedha zipo hivyo hakuna sababu ya kuona mradi huo unasuasua kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunawaadhibu watoto wetu wenyewe na pia tutakuwa tunamuangusha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Sululu Hassan kwani kama ni fedha amekwishatoa na kilichobaki ni kwetu sisi wataalamu kuhakikisha tunasimamia kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.
Aidha Mhe QS Kipanga amepata fursa pia ya kutembelea mradi wa Ujenzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam katika eneo la Kasagara ambapo amewatoa hofu wananchi na viongozi wa maeneo hapo kwa kuwahakikishaia kuwa, Mradi wa Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salamu upo pale na wasidanganywe haujawi kutolewa na wala hautatolewa katika wilaya ya Chato, ameongeza kwa kusema, “ni kweli kulikuwa na changamoto kati ya mtekelezaji wa mradi na mwenye mradi lakini hata hivyo tofauti hizo tunakwenda kuzimaliza hivi karibuni na hivyo mradi utaanza mara moja”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chato Mhe. Christian Manunga amemuomba Mhe. Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia kumpelekea salamu za dhati Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Sululu Hassan, kwani Chato sasa imepiga hatua kubwa kimaendeleo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hasa katika nyanya za Elimu, Afya na na Uchumi. Pia ametoa shukrani za dhati kwaniaba ya wilaya, ameongeza kwa kusema kwa hili la leo mimi binafsi niseme tu, “nimefa
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.