Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Chato imezishauri kamati za ujenzi kuweka wazi matumizi ya fedha na nguvu za wananchi kwenye miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa hususan ile ya inayotumia vikundi vya ujenzi (Force account).
Kamati ya Fedha imetoa ushauri huo leo tarehe 19.08.2019 wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Halmshauri ya Wilaya ya Chato.
Wajumbe hao wamezishauri kamati za ujenzi kwenye miradi mblimbali kuweka wazi fedha zote ambazo imekuwa zikipokelewa pamoja na kushirikisha viongozi na jamii husika kwa kuwapa taarifa juu ya maendeleo ya miradi hiyo.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.