Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato ndugu Mandia Kihiyo amezitaka kamati za ujenzi wa vyumba vya madarasa chini ya mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya ya UVIKO-19 kuhakikisha zinakamilisha ujenzi na kukabidhi madarasa hayo ifikapo tarehe 29 Desemba 2021.
Mkurugenzi Mtendaji ameyasema hayo leo kwa nyakati tofauti wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu hiyo katika kata za Nyamirembe, Ilemela, Kigongo, Muganza na Bwongera.
Amezipongeza kamati ambazo zimesimamia vyema na kukamilisha ujenzi ikiwemo utengenenezaji wa madawati.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.