Kamishna wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe.Magdalena Kamugisha Rwebangira akiambatana na Afisa Utumishi wa Tume hiyo Bi. Amina Lalika, Mnamo Septemba 20, 2025 walifika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa majimbo ya Chato Kusini na Chato Kaskazini Ndg. Abel Johnson Manguya kwa lengo la kukagua shughuli za maandalizi ya Uchaguzi Mkuu yanavyokwenda.
Akizungumza mara baada ya kukagua stoo ya vifaa vya Uchaguzi na kusomewa taarifa ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu, pamoja na mapokezi ya fedha, Mhe. Magdalena alimpongeza Msimamizi huyo wa Uchaguzi kwa mpangilio mzuri wa vifaa lakini pia kwa taarifa nzuri ambayo imejipambanua kwa mtiririko mzuri na kueleweka, hivyo alikiri kuipokea huku akimtaka yeye na timu yake ya Uchaguzi kuendelea kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha amani na utulivu vinatawala.
Hata hivyo baada ya kukamilisha zoezi la ukaguzi, timu hiyo iliambatana na Msimamizi wa Uchaguzi wa Majimbo hayo akiwa na Afisa Uchaguzi wa majimbo hayo Ndg. Tagaya Vedastus kuelekea kijiji cha Igarula kata ya Kasenga kufuatilia zoezi la kampeni linavyokwenda ambapo Mgombea ubunge Ndg.Cornel Lucas Magembe wa Jimbo la Chato Kaskazini alikuwa akifanya kampeni katika eneo hilo.
Ikumbukwe kuwa kauli mbiu ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ni " *Kura yako Haki yako Jitokeze kupiga kura"*
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.