Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo amewaagiza viongozi na wataalamu wilayani Chato wanaosimamia miradi ya maendeleo kuhakikisha miradi yote inakamilka kwa ubora na kwa wakati.
Ndugu Chongolo ametoa maagizo hayo leo Novemba 17, 2021 Wilayani Chato alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Chato.
Ndugu Chongolo amesema serikali imekuwa ikitoa fedha ili kutekeleza miradi lakini miradi mingi imekuwa ikichelewa kukamilika huku ikitumia gharama kubwa pasipo wataalamu kuishauri ipasavyo serikali katika kuboresha au kupunguza gharama za miradi hiyo, " fedha zikija hapa lengo zifanye kazi na zitoe matokeo ya muda mrefu, ninyi ni wataalamu saidieni kushauri kitaalamu miradi ambayo itatoa matokeo ya muda mrefu" alisema ndugu Chongolo.
Katibu Mkuu CCM pia ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Chato kuhakikisha ujenzi wa stendi mpya ya Kahumo unakamilika ifikapo tarehe 30, Disemba 2021.
"kwenye ilani ya CCM tuliahidi kumaliza hili kwa kipindi husika, tulitamani sana mradi huu utekelezwe kwa wakati na uishe kama ilani inavyosema" amesisitiza Katibu Mkuu
Katika hatua nyingine Ndugu Chongolo amewasihi wananchi ambapo miradi inatekelezwa kuhakikisha wanailinda vizuri miundombinu yote ili iweze kudumu pia kuondoa hasara inayoweza kutokana na ukarabati wa miradi hiyo.
Miradi ambayo imetembelewa na Katibu Mkuu wa CCM ni pamoja na Shule ya sekondari Mbuye, shule maalumu ya Mbuye, ujenzi wa stendi Kahumo na kituo cha afya cha Nyabilezi.
Imetolewa na Richard Bagolele-Chato
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.