Mkuu wa wilaya ya Chato mhe. Louis Peter Bura ametembelea wakulima wa zao la pamba na tumbaku januari 23/2025 katika kata ya Iparamasa Wilayani Chato.
Bura amewapongeza wakulima wa zao la pamba, ambapo amefurahishwa na jitihada wanazoendelea nazo za kuakikisha wanalima zao hilo kwa weredi na kwakufuata taratibu zote na hasa kipimo cha 60 kwa 30 na kuakikisha dawa za kuua wadudu zinanyunyuziwa kwa wakati,kwani mkulima asipopiga dawa kwa wakati wadudu watasababisha hasara.
Pia amewapongeza wakulima wa zao la tumbaku wanao fanya vizuri na amewasihi wale ambao bado wanalima zao hilo kwa mara ya kwanza, kujitahidi kuzingatia taratibu na kanuni ili kuweza kupata mavuno ya kutosha na yenye ubora.
Naye Walwa Zakaria aliye jishidia zawadi ya trekta kutoka kwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan, aliye kuwa mkulima bora wa pamba, ameahidi kuwa ataakikisha wakulima wote wanafanya vizuri ili wilaya ya Chato izidi kushamili kitaifa na kimataifa.
Na kwa wakati huo huo mkuu wa wilaya mhe. Bura ametembelea ujenzi wa shule ya sekondari Mwendakulima, sekondari ya Iparamasa na sekondari ya Kabantange, ambapo ametoa rai kwa wasimamizi wa miradi hiyo kuakikisha wanazingatia maelekezo na kuwa waamnifu katika matumizi ya fedha , kusudi miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati na kwa ubora uliotarajiwa.
"Katika wilaya yangu sihitaji kuona mradi wowote unaishia njia kwa kisingizio cha fedha kuisha! kwasababu fedha zinaletwa zikiwa zinajitoshereza kwa kila mradi husika sitaki kusikia ubadhirifu wa aina yoyote wala konakona, maana rais anatoa fedha akilenga wananchi wake kuondokana na changamoto za huduma za kijamii" asema Bura.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.