Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Chato leo imefanya ziara yenye lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri kwa mwaka huu.
Mjumbe wa kamati Mhe. Phares ambaye ni diwani wa kata ya Ilyamchele amesema wamefurahishwa na miradi hususan ule wa Ufyatuaji wa Matofali na kuishauri timu ya Menejimenti iweze kufyatua tofali zenye ubora lakini pia kwa gharama nafuu ili kila mwananchi na taasisi ziweze kununua tofali hizo na mradi uwe endelevu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Mhe. Christian Manunga akiwa kwenye mradi wa Soko la kimataifa la Kasenda amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha anatengeneza mazingira mazuri katika soko hilo ikiwa ni pamoja na kuziba mashimo yaliyopo katikati ya soko hilo pamoja na utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara katika soko hilo.
Miradi mingine iliyotembelewa na kamati hiyo ni pamoja na ujenzi wa kituo kipya cha mabasi cha Muganza pamoja na ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu uliopo kijiji cha Mlimani kata ya Muungano.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.