Kauli hiyo imetolewa na Mhe. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Chato Ndg. Barnabas Nyerembe katika Kikao Maalumu kilichofanyika Januari 22, 2023 katika Ofisi za Chama.
Akizungumza na wajumbe wa Mkutano huo Mhe. Nyerembe amesisitiza kuwa lengo la Kikao hicho Maalumu ni kufanya Majadiliano dhidi ya Changamoto zinazokwamisha ukusanyaji na kuweka mikakati juu ya ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri kwa asilimia 100
Aidha kikao hicho kiliwahusisha wajumbe wa kamati ya siasa wilaya pamoja na Timu ya Menejimenti kutoka Halmashauri ambapo kwa kauli moja wamekubaliana kila mmoja kwenda kutimiza wajibu wake katika kusimamia ukusanyaji wa mapato ya halmashauri.
Pamoja na kuwepo kwa wajumbe wa kamati ya siasa, timu ya menejimenti pia watendaji wa kata walipata fursa ya kuelezea changamoto wanazokutana nazo katika ukusanyaji wa mapato ambazo kwa pamoja zilijadiliwa na kutolewa ufafanuzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chato Ndg. Mandia Kihiyo ameahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa kila hatua ili mapato ya Halmashauri yaweze kukusanywa kwa asilimia 100 ikiwa ni pamoja na kutoa mahitaji mhimu kwa ajili ya kukusanya mapato ikiwa ni pamoja na kulipa asilimia 5 ya wakusanya mapato kwa wakati pamoja na uwepo wa mafuta kwa ajili ya timu za ufatiliaji mda wote.
Katika hatua nyingine kwa upande wake Mkuu wa wilaya Chato ambaye alipata fursa ya kuzungumza na wajumbe wa kikao hicho, aliahidi ofisi yake itakwenda kusimamia yale yote yaliyojadiliwa ikiwa ni pamoja na kwenda kuzungumza na TRA, ofisi za NIDA ili vile vikwazo wanavyokutana navyo katika ukusanyaji wa Lesseni unapatiwa ufumbuzi.
Akihitimisha Mhe. Mkuu wa wilaya amewashukuru watumishi wote kwa namna ambavyo tumeshirikiana kwa mwaka 2023 na kuomba ushirikiano na upendo uzidi kuimarishwa kwani ndio msingi wa maendeleo na ufanisi.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.