Mawaziri 8 wakiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wamefika Wilayani Chato kwa lengo la kutatua migogoro ya rdhi katika hifadhi za misitu.
Akitoa taarifa ya Wilaya kwa msafara huo, Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri amesema kwa Wilaya ya Chato kata ya Bwanga, Iparamasa, Butengorumasa, Buziku, Nyarutembo, Kasenga na Bwongera zinao wakazi wengi ambao wanafanya shughuli za kiuchumi katika hifadhi za misitu hiyo ikiwemo kilimo na ufugaji.
Amesema kutokana na ukuaji wa miji inayopakana na hifadhi hususan kata ya Bwanga ni dhahiri kuwa kunahitajika ardhi kubwa kwa ajili ya uendelezaji wa mji huo ikiwemo ujenzi wa taasisi na maeneo ya viwanda.
Akiongea na wananchio waliokusanyika shule ya sekondari Magufuli waziri Lukuvi amesema amesikiliza kero za wananchi wa Chato na Bukombe kuhusiana na uhaba wa ardhi na kuhaidi kufikisha kero hizo kwa mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mawaziri wengine walikuwepo kwenye msafara huo ni pamoja na Waziri wa nchi ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamis Kigwangala, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe, Husen Mwinyi, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa, Naibu waziri wa Kilimo na naibu waziri ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.