Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe.Louis Bura,ametembelea banda la Chato kwenye Maonesho ya 8 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika Mkoani Geita kwenye Viwanja vya Dr.Samia Suluhu Hassan,na kufurahishwa na bidhaa za Asali,Mafuta,Sabuni,Nishati safi ya kupikia na Samani, na kuwapongeza kwa juhudi za kufanya kazi nzuri na yenye tija kwa maisha yao na Taifa.
Mhe Bura amewaagiza wataalamu wa Halmashauri kuwatembelea mara kwa mara wajasiriamali hao na kuwapa ushauri na mafunzo ili kuboresha bidhaa zao ,ili waweze kukidhi viwango vya kimataifa vya kiushindani. ” Maonesho haya tunakoelekea yatakuwa ya Kimataifa hivyo ushindani wa bidhaa utakua mkubwa, kwahiyo nawaomba sana wataalamu muwajengee uwezo na kuwapa ushauri ili waweze kukua na kuweza kushindana na wajasiriamali kutoka mataifa mbalimbali”.
Maonesho hayo yanayofanyika Mkoa wa Geita kwa mara ya 8 mfululizo mwaka huu yamebeba kauli mbiu “ Ukuaji wa Sekta ya Madini ni Matokeo ya Matumizi ya Teknolojia sahihi na Uongozi bora, Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025”.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.