Mwenyekiti wa wazazi Taifa Mhe.Fadhiĺ Rajabu Maganya amekuwa na ziara ya kikazi mkoani Geita akitembelea na kukagua miradi ya mendeleo katika wilaya zote za mkoa kunzia 10, Machi 2024 na kuihitimisha wilayani Chato mnamo 14 mchi 2024, ambako alifurahishwa na mshikmano uliopo baina ya viongozi wa chama na serikali.
Akiwa wilayani Chato Mhe. Maganya ametembelea na kukagua mradi wa shule ya sekondari Kabantange iliyopo kata ya Bwanga, Mradi wa Maji unaotekelezwa chini ya usimamizi wa RUWASA katika kijiji cha Bwanga unaotarajia kusambaza maji katika vijiji vya na Bwanga, ameweka jiwe la Msingi ujenzi wa nyumba ya Mwenyekiti wa Wazazi Chato, pia ametembele Hospitali ya Kanda Chato na kujionea huduma mbalimbali za afya zinavyotolewa hospitalini hapo.
Akizungumza katika kikao cha majumuisho kilichofanyika katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA hapa Chato Mhe. Maganya aliyasema hayo baada ya kupokea taarifa ya wilaya ya Chama na Serikali.
Aidha Mhe. Maganya ameupongeza uongozi wa wilaya kwa namna ambayo unaendelea kusimamia na kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM kupitia miradi inayotekelezwa ndani wilaya hasa katika sekta za Elimu, Afya na Maji kwani ndio zinazogusa kundi kubwa la wananchi.
Sambamba na hilo Mhe. Maganya amewaasa viongozi kila mmoja katika eneo lake kujenga utamaduni wa kusikiliza kero za wananch wanaowahudumia katika maeneo yao.
Akitoa salamu za shukrani Mhe. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Geita, Ndg. Nicholaus Kasindamila amemhakikishia Mhe. Maganya kuwa Chama na Serikali ndani ya mkoa kiko salama na kinafanya kazi vizuri kwa kushirikiana na Wataalamu bila shida yoyote, huku akiahidi kwenda kuzishughulikia changamoto ndogondogo ambazo zinataka kuchafua taswira na uhai wa Chama chetu, ameongeza kwa kusema, "ndugu zangu hizi ni changamoto kati ya mtu na mtu wala siyo chama au Serikali"
Mhe. Mkuu wa mkoa wa Geita Ndg. Martine Shigela aliyewakilishwa na Mhe. Mkuu wa wilaya ya Chato Ndg. Said Nkumba amempongeza Mhe Maganya kwa ziara aliyoipanga na kuifanya ndani ya mkoa wa Geita kwani imekuwa chachu na yenye tija
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.