Halmashauri ya Wilaya ya Chato leo tarehe 16.11.2020 imetoa mikopo kwa vikundi 29 vya wanawake 18, vijana 9 na wenye ulemavu viwili yenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 116.Miongoni mwa vikundi hivyo vimekabidhiwa vifaa ikiwemo pikipiki, mashine ya kusaga, mashine ya kutotoleshea vifaranga, vifaa vya uvuvi na mashine ya kutengeneza viatu. Akiongea katika hafla ya Makabidiano ya mikopo na vifaa hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Chato mhandisi Charles Kabeho amevitaka vikundi hivyo kuheshimu mikopo hiyo ikiwa ni pamoja na kurejesha kwa wakati ili vikundi vingine pia viweze kukopa
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.