Na Richard Bagolele-Chato
Shirika la hifadhi ya Taifa (TANAPA) limedhadhili Wilaya Chato ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, ofisi ya walimu wa shule mpya ya sekondari ya Kikumbaitale iliyopo kata ya Kigongo pamoja na Boti yenye injini kwa kijiji cha Mwekani vyote vikiwa na thamani ya Shilingi milioni 99.
Akikabidhi miradi hiyo kwa Mkuu wa mkoa wa Geita mwenyekiti ya Bodi ya wadhamini ya TANAPA Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara ameitaka jamii kuitunza miradi hiyo ili iweze kuleta manufaa kwa wananchi wa kata ya Kigongo hususan kijiji cha Kikumbaitale.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt. Allan Kijazi amesema mradi wa vyumba vya madarasa umetekelezwa kwa ushirikiano wa TANAPA kupitia hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo na wananchi wa kijiji cha Kikumbaitale kata ya Kigongo ambapo TANAPA ilitoa kiasi cha shilingi milioni 46 na wananchi wa kijiji cha Kikumbaitale wamechangia vifaa kama vile mawe,kokoto, mchanga , tofali na maji ambavyo vimekadkugharimu juml a ya shilingi milioni 6.
Aidha Dkt. Kijazi amesema TANAPA imeamua kufadhili boti ya kisasa yenye injini na maboya yenye thamani ya shilingi milioni 47 kwa kikundi cha kusimamia fukwe cha Mwelani (BMU) ya kijiji cha Mwelani kutokana ushirikiano wa kijiji hicho na hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo katika kupambana na uvuvi haramu ndani ya ziwa Viktoria “ ni kutokana na ushirikiano huo TANAPA kupitia hifadhi kisiwa cha Rubondo ilipokea na kupitisha maombi toka kwa wananchi wa kijiji cha Mwelanina kuwapatia mradi wa Boti, injini na maboya yake ambayo itatumika kufanya doria katika ziwa Viktoria.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Eng. Robert Gabriel ameishukuru TANAPA kwa ufadhili wa miradi hiyo na kuahidi kuwa mkoa itasimamia vyema miradi hiyo. Aidha Mkuu wa mkoa wa Geita amewataka wakazi wa Chato kuendelea kutoa taarifa za kuhusiana na uvuvi haramu. Ameagiza wananchi wote kwa kushirikiana na viongozi kufanya msako wa nyumba hadi nyumba ili kubaini nyavu haramu ambazo bado hazijasalimishwa.
Bodi wa wadhamini ya TANAPA ipo mkoani Geita kwa ajili ya vikao vya bodi hiyo ambavyo vinafanyika kwenye hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo. Wakiwa Wilayani Chato wajumbe wa bodi ya wadhamini ya TANAPA walipata fursa ya kutembelea uwanja wa ndege wa Chato ambapo wamesema kukamilika kwa uwanja huo utasaidia kuibua fursa nyingi za kiuchumi na kuongezeka kwa idadi ya watalii kufika hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo na hifadhi zingine zilizo jirani hasa katika mkoa wa Kigoma.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.