Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela akikagua Miradi wa Ujenzi wa Shule Mpya katika kijiji cha Ipandikilo inajengwa kwa fedha za Serikali wenye thamani ya shilingi Milioni 400 kwa kila shule na zinajengwa shule mbili mpya ukiwa na lengo la kumaliza kabsa adha ya mrundikano wa wanafunzi wa shule za msingi kwenye kata ya Makurugusi na Kachwamba wilayani Chato mkoani Geita.
Mhe. Shigela ameipongeza Halmashauri ya wilaya kwa usimamizi mzuri wa ujenzi katika wa shule hizo, Shule hizo ni mpango mkakati wa serikali wa kupunguza msongamano wa wanafunzi pamoja na kuinua taaluma kwa wananfunzi waliopo wilayani humo.
Aidha Mhe. Shigela ametoa pongezi hizo baada ya kukagua ujenzi wa shule mpya ya Kaseni iliyopo kata ya Kachwamba ambayo inatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi milioni 400 kukamilika kwake.
Hata hivyo Mhe. Shigela amesisitiza uadilifu katika ujenzi na usimamizi wa miradi ya umma,sambamba na kuwalipa kwa wakati wakandarasi na mafundi katika ujenzi huo kutokana na kile alichodai kuwa fedha za miradi hiyo zipo.
Ameongeza kwa kusema, "watu waliamini kuondoka kwa Hayati Magufuli ndiyo ingekuwa mwisho wa maendeleo kwenye wilaya yetu na mkoa wa Geita...nataka niwahakikishie kuwa dhamira ya Mheshimiwa Rais Samia ni njema ya kuhakikisha yale yote yaliyoanzishwa na Hayati Magufuli na yeye akiwa Makamu wa Rais maana yake walikuwa wanafanya kama timu moja yanakamilika"
"pia yale ambayo yalikuwa hayajaanzishwa lakini ni kero ya wananchi mheshimiwa Rais Samia anashughulika nayo...na miongoni mwa hayo ni pamoja na ujenzi wa shule hii ya msingi...kwahiyo niwapongeze sana kwa kupata milioni 400 kujenga shule mpya hii ya kisasa kwaajili ya shule ya msingi" amesema Shigela.
Awali Mhe. Mkuu wa wilaya ya Chato Eng. Deusdedith Katwale amesema fedha hizo zimetoka serikali kuu na Halmashauri imekuwa mstari wa mbele kuzisimamia ili mradi yote ikiwa ni pamoja na mradi huu unakamilika bila kukwama sehemu yoyote.
Aidha tumekubaliana na Halmashauri ya wilaya kuwa na Kamati ndogo za Usimamizi wa Miradi ya Ujenzi kutoka Serikali za vijiji lengo likiwa ni kuhakikisha Miradi yetu yote ndani ya wilaya inakuwa na ubora na kiwango kinachotakiwa pia amewashukuru wananchi kwa kutoa ushirikiano mkubwa wanaoendelea kuuonyesha katika miradi mbalimbali.
Mhe. Diwani wa Kata ya Kachwamba Ndg. Stella Masabile akizungumza kwa niaba ya wananchi ameelezea changamoto wanazokabiliana nazo licha ya ujenzi huo kufikia aslimia 50 ni kupanda kwa gharama za vifaa vya ujenzi na ubovu wa miundo mbinu ya barabara unaochangia kuchelewesha ujenzi huo kutokana na vifaa kutofika kwa muda mwafaka.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.