Akiongea na wanachi wa Bwanga Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Geita Ndg. Martine Shigella katika Hafla ya utiaji saini juu ya utelezaji wa Mradi huo, uliofanyika katika viwanja wa Shule ya Sekondari Kabantange iliyopo katika kata ya Bwanga ambapo Mhe. Shigela ameshuhhudia utianaji saini wa mikataba yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 4 ikiwa ni utekelezaji wa miradi kaika wilaya za Chato, Bukombe na Nyang’wale ambazo zinapatikana mkoani Geita.
Aidha Mhe. Martine amewakumbusha wakandarasi waliopata kazi hizo kufanya kazi hizo kwa uzalendo kwani Mhe. Rais anazitafuta fedha hizo kwa shida hivyo kila mtanzania anaepata fursa ya kufanya kazi kwa ajili ya wengine basi ni imani yangu kuwa atatimiza wajibu wake kwa ukamilifu na ubora wa hali ya juu.
Pia Mhe. Martine ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Chato kwa kusimamia vizuri miradi ya Maendeleo ambayo si tu kwa kuitazama bali hata ubora wake ni wa kiwango cha hali ya juu.
Kwa upande wake msimamizi wa utekelezaji wa Mradi huo Eng. Exsavery ambaye ni Meneja wa Ruwasa wilaya ya Chato amesema, “ mradi huu ni mkubwa na utanufaisha zaidi ya wakazi elfu ishirini na nane na umeandaliwa kuwa suruhisho kwa wakazi wa Bwanga na Vitongoji vyake kwa zaidi ya miaka ishirini ijayo”
Hata hivyo Eng. Exsavery amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji ndani ya wilaya ya Chato.
Mradi unatekelezwa na Mkandarasi Otonde chini ya usimamizi wa Ruwasa Chato ambapo mda wa utekelezaji ni miezi 8 na katika Mradi huo Mkandarasi atakuwa kazi ya kujenga tenki la lenye ukubwa wa ujazo wa lita 2250,000, ‘Pump House 2, vituo vya kutolea maji 17, Ofisi 1 kwa ajili ya Mradi pamoja na thamani zake ikiwa ni pamoja na kompyuta.
Mkuu wa wilaya ya Chato Mhe. Deusdedith Katwale akitoa salamu za wilaya amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa dhati katika kuhakikisha wananchi wa Bwanga na Chato kwa ujumla wanakuwa na maisha bora ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanapata maji safi na salama ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2020 hadi 2025 yenye lengo la kuhakikisha ifikapo 2025 mtanadao wa Maji uwe umewafikia wananchi kwa asilimia 85
Aidha Mhe. Katwale amewaomba wananchi wa Bwanga kukaa mkao wa kula kwani ule Mradi wa Ujenzi wa Stand ya Mabasi Bwanga unakwenda kuanza utekelezaji wake mda wowote kuanzia sasa kwani mgogoro uliokuwepo kati ya TBA na Halmashuri umepatiwa ufumbuzi.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.