Mwakilishi wa Ubalozi wa Japan nchini Tanzania Ms. Nanae Takeda, Jana Novemba 3, 2023 alifanya ziara ya kukagua miradi mitano ya maendeleo yenye thamani ya Tsh. 920,228,566/= ambayo imefadhiliwa na Ubalozi wa Japan nchini Tanzania.
Miradi hiyo ni Matengenezo ya barabara kiwango Cha lami Muganza - Kasenda (0.5 Km), Ujenzi wa Soko la kimataifa la samaki Kasenda, Ujenzi wa vitalu nyumba 8 (Greenhouses) Nyabilezi, Ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na matundu 22 ya vyoo shule ya msingi Idoselo, Pamoja na vyumba viwili vya madarasa na matundu 20 ya vyoo shule ya msingi Nyambogo.
"Nimetembelea miradi yote mitano tuliyoifadhili na nimeiona, kazi mliyoifanya ni kubwa na nzuri sana hivyo mnastahili pongezi, Ahsanteni sana" Alisema Nanae Takeda.
Naye Mkuu wa wilaya ya Chato Mhe. Mhandisi Deusdedith Katwale akizungumza Kwa niaba ya wananchi wa wilaya hiyo aliwashukuru saana Ubalozi wa Japan nchini Tanzania na kuahidi kuwa miradi hiyo italindwa na kutunzwa Kwa nguvu zote kwani imeweka alama kubwa na manufaa Kwa wananchi, hivyo aliwaomba uhusiano huu mzuri uwe wa kudumu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Ndg Mandia H. Kihiyo wakati akimkabidhi Ms. Nanae Takeda HATI YA SHUKRANI aliupongeza sana Ubalozi wa Japan nchini Tanzania Kwa kufadhili miradi hiyo mitano hapa wilayani, ambayo imeleta mabadiliko makubwa hususani ya kiuchumi katika jamii jambo ambalo wananchi wa Chato wataendelea kuwakumbuka daima.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.