Jumla ya miradi 11 yenye thamani ya shilingi milioni 944,020,000 imezinduliwa, kuwekewa jiwe la msingi na kutembelewa na Mwenge wa Uhuru 2018 Wilayani hapa.
Akizindua miradi hiyo kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 ndg. Charles Francis Kabeho ameipongeza Wilaya ya Chato kwa kuwa na miradi mizuri yenye kuzingatia thamani ya fedha.
“Niwapongeze viongozi wa Wilaya hii kwa miradi mizuri changamoto kwetu ni kuitunza ili iweze kutoa huduma kama ilivyokusudiwa” alisema kiongozi wa Mbio za Mwenge.
Wakizindua Bwalo la Chakula la sekondari ya Magufuli mbali na kufurahishwa na ubora wa bwalo hilo viongozi hao wameomba jitihada za kujenga jiko la kupikia la shule hiyo zifanyike haraka ili wananfunzi waweze kupata huduma bora ya Chakula. Katika kuunga mkono kiongozi wa mbio za Mwenge WA Uhuru na timu yake walichangia mifuko 6 ya saruji ili kuwezesha ujenzi huo, Mbunge wa Jimbo la Chato na Waziri wa Nishati mhe. Dkt. Medard Kalemani naye alichangia mifuko 30 ya saruji pamoja na viongozi wengine wa Halmashauri nao walichangia.
Akikabidhi Mwenge wa Uhuru 2018 mkoani Kagera Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amesema jumla ya miradi 63 yenye thamani ya shilingi bilioni 12.7 imepitiwa na Mwenge wa Uhuru Mkoani Geita huku miradi mitano ikishindwa kuzinduliwa kutokana na kutofautiana kwa thamani ya miradi hio na taarifa zilizopo ofisi ya mkuu wa Mkoa Geita ambapo amesema uchunguzi wa suala hilo unaendelea.
Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge 2018 ni elimu ni ufunguo wa maisha wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.