Mkuu wa wilaya ya Chato Mhe. Deusdedith Katwale ameyasema hayo mapema hii leo katika ufunguzi wa utelelezaji wa mradi wa WASH na SWASH kwa mwaka wa fedha 2021/2022 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri chenye lengo la kupeana taratibu na vigezo mbalimbali ili mradi huo utekelezwe kwa viwango na ubora unaotakiwa.
Aidha kwa nyakati tofauti Mhe Katwale akizungumza na wajumbe wa mkutano huo amesisitiza sana juu ya uwajibikaji hasa katika usimamizi wa Miradi ya Maendeleo kwani Serikali na Taifa kwa ujumla imetuamini na kutupa dhamana hii kubwa ya kusimamia utekelezaji wa mradi huu hivyo kila mmoja aende akatimize wajibu wake kwa kuzingatia sheria na taratibu za utekelezaji wa mradi.
Afisa Afya wilaya ya Chato Bi Fransisca akitoa taarifa fupi juu ya mradi kwaniaba ya Mkurugenzi Mtndaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chato Bw. Mandia Kihiyo amewataka wajumbe wote wa kikao kwenda kuwa mabalozi wazuri katika kuhakikisha yale yote tuliyopitishwa na wataalamu juu ya utekelezaji wa mradi huu yanafikiwa kwani mradi huu unatekelezwa na Bank ya Dunia kupitia lipa kwa matokeo.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.