Kauli hiyo ameitoa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chato Ndg. Mandia Kihiyo mapema hii leo alipokuwa akikabidhi pikipiki 7 zilitolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa ajili ya Watenda wa Kata katika viwanja vya Makao Makuu ya Halmashauri.
Aidha Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu Ndg. Martine Ndamo akitoa neno kabla ya pikipiki hizo kukabidhiwa kwa watendaji wa Kata amewataka Watendaji wa Kata kutambua kuwa pikipiki hizo watakazowagawia leo na Mkurugenzi Mtendaji ni awamu ya kwanza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amewapatia pikipiki hizi ili muende mkaboreshe utendaji kazi katika maeneo yenu" na kama mnavyojua sisi kama Halmashauri tuna kata 23 hivyo kadri zikakavyokuwa zinakuja tutawagawia ili kila Mtendaji awe na pikipiki yake na hiyo ndo adhima ya Serikali.
Pia Ndg. Ndamo amewataka watendaji wa Kata kwenda kutumia vyombo hivyo kwa umakini mkubwa ikiwa ni pamoja na kuzitunza. Pia amesisitiza kwa kusema, "watumishi wenzangu pikipiki hizi mnazopewa leo ni mali ya Serikali asitokee mtu akajimilikishe na hata ukiondoka au kuhama pikipiki hii ibaki ni mali ya Ofisi ya Mtendaji wa Kata"
Akikabidhi pikipik hizo Mkurugenzi Mtendaji Bw. Mandia kwanza amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ameendelea kuboresha maslahi na mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi na leo tunaona pikipiki hizi ambazo zimetolewa nchi nzima lengo lake likiwa ni kuboresha na kurahisisha utendaji kazi kwa Afisa Mtendaji wa Kata.
Ndg.Mandia amesisitiza matumizi sahihi ya pikipiki ili zikalete tija katika maeneo ya kazi hasa katika nyanja za utoaji wa huduma bora kwa wananchi mnaowahudumia, usimamizi wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katka maeneo hasa katika sekta ya Elimu, Afya na Maji pamoja na ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.
Kwa upande wa Watendaji wa Kata waliopewa pikipiki hizo wametoa shukrani nyingi kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. Samia kwa kumuahidi kwenda kutenda kazi kwa weledi na uaminifu mkubwa .
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.